al-Fawzaan kuhusu kumpa mtoto jina la Luutw

Swali: Kuna wanaowaita wavulana wao kwa jina la Luutw akifanya hivo kwa kukusudia kuwakumbusha watu fedheha ya tendo la liwati. Je, kitendo chake ni sahihi?

Jibu: Vipi? Anamwita Luutw kwa sababu ya kuwatahadharisha watu na liwati? Haya ni maoni ya ajabu. Amwite Luutw kwa sababu ni Nabii na si kwa sababu ya uliwati. Amwite kwa sababu ni jina la Nabii mtukufu. Luutw, Nuuh na Ibraahiym, haya ni majina ya Manabii (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam).

Luutw (´alayhis-Salaam) aliitwa kwa jina hili kabla ya Allaah Kumtuma kwa kundi hili.

فَآمَنَ لَهُ لُوطٌ

“Basi Luutw akamwamini.” (29:26)

Hapa ni katika ardhi ya Iraaq. Kabla ya yeye kuhama kwenda katika ardhi ya Shaam alikuwa anaitwa Luutw tokea asli. Haina mnasaba wowote kwa kutumwa kwa wanaliwati. Lisiambatanishwe kati ya hili na hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 17/08/2020