al-Fawzaan kuhusu anayotazama mposaji kwa anayetaka kumposa 

Swali: Ni lipi jambo lililowekwa katika Shari´ah kwa mchumbiaji anapomtazama mchumba wake; atazame uso peke yake au yale anayoona mwanaume kwa Mahram wake bila ya kuwa na ´Abaa´ah na mtandio nikiwa na maana ya kwamba awe kichwa wazi?

Jibu: Ni sawa. Amtazame uso wake, vitanga vyake na nywele za kichwani mwake kwa sababu anaweza kuwa na kasoro kwenye nywele za kichwani. Ni sawa akatazama nywele za kichwani mwake, uso wake na vitanga vyake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 17/08/2020