al-Fawzaan kuhusu kujitolea kiungo kumpa kafiri

Swali: Inajuzu kumpa kiungo miongoni mwa viungo vya mwili kafiri anayehitajia?

Jibu: Ndio. Kama jinsi unavyoweza kumlisha anapohitajia na kumfanyia wema, kadhalika [hili] ni sawa. Kwa sharti asidhurike yule mwenye kutoa kiungo hichi. Ni sawa ikiwa unaweza kukitoa na hilo lisikudhuru. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ

“Na fanyeni wema; kwani hakika Allaah anapenda wafanyao wema.” (02:195)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amefaradhisha kufanya wema juu ya kila kitu.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (75) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-11-05.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020