Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa hatuna haja ya kusoma madhehebu ya Mu´tazilah na Jahmiyyah na mfano wao kwa kuwa ni mapote yemeondoka…

Jibu: Hatuyasomi kwa kuwa tuna haja nayo. Tunayasoma tuyajue ili tuweze kujiepusha nayo na kuyatahadharisha. Vinginevyo hatuna haja nayo. Sisi tumetosheka na Qur-aan na Sunnah na yale waliyokuwemo Salaf wa Ummah huu. Sisi hatuyasomi kwa kuwa tuna haja nayo. Bali tunayasoma kwa kuwa tuna haja ya kuyajua ili yasiwaingilie watu na tuyatahadharisha na khaswa ukizingatia ya kwamba [madhehebu haya] leo yana walinganizi ambao wanalingania kwayo. Walinganizi hao wanachapisha vitabu vya Mu´tazilah, wanavikagua na kuvieneza. Ikiwa hatujui madhehhebu yao na utata wao, pengine yakatuingilia au kwa wale watu wetu ambao ni wajinga. Hili ni lazima kwetu. [Mshairi anasema]:

“Yule asiyejua shari hutumbukia ndani yake.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (76) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-11-12.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020