al-Barbahaariy aliwasusa Ahl-ul-Bid´ah kwa mkono na mdomo wake

149- Sharh-us-Sunnah

Imeandikwa na al-Barbahaariy. Anaitwa Abu Muhammad al-Hasan bin ´Aliy bin Khalaf al-Barbahaariy. al-Barbahaariy ni unasibisho wa matibabu ya kihindi yanayoitwa “Barbahaariy”. Aliyekuwa akiyaleta alikuwa anaitwa “al-Barbahaariy”.

Alikuwa ni mwanachuoni mkubwa wa madhehebu ya Hanaabilah. Alikuwa anaishi Baghdaad na huenda pia alizaliwa huko. Alifariki 329.

Ibn Abiy Ya´laa amesema juu yake:

“Alikuwa ni Shaykh wa Hanaabilah katika zama zake. Alikuwa ndio mtu wa kwanza kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah na kuwasusa kwa mkono na mdomo. Alikuwa na sifa nzuri kwa mtawala na manzilah nzuri kwa Hanaabilah. Alikuwa ni mmoja katika maimamu waaminifu wenye kumjua Allaah na wenye kuhifadhi misingi kwa njia inayotakikana.”

adh-Dhahabiy amesema:

“Alikuwa Faqiyh na kiigizo na Shaykh wa Hanaabilah Iraaq kwa njia zote. Alikuwa na sifa kubwa na cheo kitukufu.”

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taariykh Tadwiyn-il-´Aqiydah as-Salafiyyah, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 06/09/2020