Imaam al-Albaaniy: Mimi nataka kusema kuhusiana na maneno ya Shaykh Hamiyd – Allaah amjaaze kheri – kuhusu baadhi ya kazi za Shaykh al-Qaradhwaawiy na kwamba ana mfumo mmoja kama wa al-Ghazaaliy. Kama kwamba watu hawa walisoma pamoja na wana fikra moja.
Mwanafunzi: al-Qaradhwaawiy anamchukulia al-Ghazaaliy kama mwalimu wake.
Imaam al-Albaaniy: Kweli?
Mwanafunzi: Ni mdogo kwake kiumri.
Imaamal-Albaaniy: Ni sahihi. Lakini hawana tofauti kubwa kati yao.
Mwanafunzi: Kuna tofauti Shaykh. Si chini ya miaka kumi kati yao.
Mwanafunzi: Shaykh al-Ghazaaliy ana miaka 78.
Sawa. al-Qaradhwaawiy ana miaka mingapi? Kwa kuwa kuna kipindi niliishi Qatar. Na nilikuwa nikikutana na al-Qaradhwaawiy na al-Ghazaaliy. Sikuona tofauti kubwa hiyo. Lakini nilichoona ni kuwa walisoma pamoja. Nukta hapa ni kuwa, wanaafikiana kwa mfumo unaokwenda kinyume na Sunnah. Unaona al-Ghazaaliy akielezea Hadiyth kwamba ni dhaifu, unamuona al-Qaradhwaawiy akifanya hali kadhalika kuwa ni dhaifu na kinyume chake. Wamekubaliana katika kuzihukumu Hadiyth nyingi ambazo ni sahihi kuwa ni dhaifu. Miongoni mwanzo ambayo ni maarufu sana ni Hadiyth iliyopokelewa na al-Bukhaariy. Hadiyth ambayo leo imekuwa kama njia ya kujua ni nani ambaye kapinda katika Sunnah. Kwa kuwa Hadiyth hii inaponya maradhi ya sasa na watu wanakimbia nyuma yake na matamanio yao. Yule ambaye anajua ya kwamba dini inapambana na maradhi haya, anasema: “Laa hawla wa laa quwwata illa biLlaah.” Na yule ambaye amepinda katika Sunnah, anajaribu kuamsha maradhi haya kwa kusema hakuna neno. Ninamaanisha Hadiyth ambayo iko kwenye [Swahiyh] al-Bukhaariy:
“Kutajitokeza katika Ummah wangu watu watakaohalalisha uzinzi, hariri, pombe na alama za nyimbo…”
al-Ghazaaliy amepuuza kabisa Hadiyth hii. al-Qaradhwaawiy amefanya hali kadhalika na tena zaidi. Ametaja maneno ya Ibn Hazm adh-Dhwaahiriy kuhusiana na Hadiyth ya kwenye al-Bukhaariy ya kwamba ni Hadiyth iliyozushwa. Haya hayasemi mtu ambaye anajua anachokisema. Kwa kuwa Hadiyth iliyozushwa – kama ndugu zangu wanavyojua – ni Hadiyth ambayo iliyosimuliwa na mtu muongo. Na je, katika Swahiyh al-Bukhaariy kuna waongo? Kamwe! Isitoshe, Hadiyth hii imepokelewa kwa njia nyingi kinyume na njia ya al-Bukhaariy ambayo ameshikamana nayo kwa ushupavu na kuikosoa. Anakuja al-Qaradhwaawiy naye anajua upokezi wa al-Bukhaariy wa Hadiyth hii na anajua wanachuoni wameipokea kwa njia nyingi wakati walimradi Ibn Hazm. Hata hivyo, akapuuza juhudi zote hizi za kielimu na kusema:
“Ibn Hazm amesema ni Hadiyth iliyozushwa.”
Hii ni dalili ionyeshayo ya kwamba anataka kukabiliana na wakati wa kisasa. Anataka Uislamu ukabiliane na matamanio ya zama hizi. Mara nyingi anatumbukia katika haya na yaonekana kuna propaganda nyuma ya hili. Allaah ndiye mwenye kutakwa msaada. Tunamuomba Allaah aihuishe Sunnah.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (823)
- Imechapishwa: 23/07/2020

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (823)
Imechapishwa: 23/07/2020
https://firqatunnajia.com/al-albaaniy-kuhusu-mfumo-wa-al-qaradhwaawiy-%e2%80%82%e2%80%82%e2%80%82%e2%80%82/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)