Upotevu wa wazi katika “Fiqh-us-Siyrah” cha al-Ghazaaliy

Kuhusiana na kitabu cha al-Ghazaaliy “Fiqh-us-Siyrah”, nimeona ya kwamba kina upotevu wa wazi. Mfano wa hilo ni kuwa anadharau mtandio. Anasema katika dibaji ya kwamba ameona jinsi wanawake al-Madiynah wanavyotembea kama kwamba wamebeba mahema.

Hali kadhalika hajali miujiza ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anasema kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya yule asiyeamini kuwa kitu kisichokuwa na uhai kiliongea na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yule asiyeamini.

Tofauti iko wazi kabisa. Hata hivyo kunakhofiwa ukafiri juu ya mtu ambaye anakanusha miujiza sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna mpaka watu ambao waliomuamini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ya miujiza yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Makhraj min al-Fitnah, uk. 170
  • Imechapishwa: 23/07/2020