al-Albaaniy kuhusu malengo ya USA katika vita vya Ghuba

Swali: Imesemekana kuwa umesema kwamba ni wajibu kwenda katika Jihaad na ndugu wa Iraaq. Je, ni sahihi?

Jibu: Yote mawili. Hatusemi kuwa kuna Jihaad ya Kishari´ah huko. Hata hivyo ina maana ya kuwatetea wananchi wa Iraaq ambao wamevamiwa na hawa makafiri.

Siku zote tunasema kwamba ni Iraaq ndio ilivamia Kuwait. Wakati mavamizi haya yalipotokea nchi za kikafiri na USA na Uingereza kwa masikitiko makubwa zikiongozwa na baadhi ya nchi za Kiislamu ili kuirudisha Kuwait kuwa huru kwa watu wa Kuwait, hapo ndipo kulifichuka ukweli wa khatari sana. Malengo ilikuwa ni kuwatokomeza wananchi wa Iraaq wote. Malengo haikuwa kwa maaskari wa Iraaq, tusisemi kundi la Ba´th, tusisemi Saddaam Husayn. Malengo ilikuwa ni wananchi wote wa Iraaq.

Kwa ajili hiyo tunasema ni wajibu kwa nchi zote za Kiislamu kuwasaidia wananchi wa Iraaq na kuwaokoa mavamizi haya yasiyokuwa na hisia na ya dhuluma.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (339)
  • Imechapishwa: 22/04/2015