Swali: Ni upi usahihi wa kusema kuwa fulani ana ´Aqiydah ya Salaf na Manhaj ya al-Ikhwaan? Je, Manhaj sio katika ´Aqiydah? Je, mgawanyo huu ulikuwepo wakati wa Salaf?

Jibu: Havitofautiana. Haiwezekani akawa ni Salafiy-Ikhwaaniy. Hata hivyo anaweza kuwa ni Salafiy katika baadhi ya vipengele na Ikhwaaniy katika vipengele vingine na kinyume chake. Pamoja na hivyo ni jambo lisilowezekana akawa ni Salafiy anayewafuata Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hiyo nyingine.

al-Ikhwaan al-Muslimuun wanalingania. Wanalingania katika nini? Je, walingania katika Da´wah ya Salaf-us-Swaalih ikiwa tutasema kuwa kuna mtu ambaye ni Ikhwaaniy-Salafiy? Hapana. Hivyo basi, huyu si Salafiy. Lakini katika baadhi ya vipengele anaweza kuwa hivo.

al-´Ubaylaan: Nilikupigia simu na nikakuuliza swali kwenye simu. Ukanambia nisiwajali wale ambao wanachanganya baina ya Manhaj ya Salaf na Manhaj ya al-Ikhwaan na kwamba hawajakuwa si Salafiyyuun wala Ikhwaaniyyuun.

al-Albaaniy: Ni kweli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (751)
  • Imechapishwa: 22/04/2015