Hapana shaka kwamba Imaam ash-Shawkaaniy ni imamu na Mujtahid akiwa na elimu iliyobobea katika elimu ya Fiqh. Alikuwa ni Mujtahid mpaka katika ´Aqiydah na sio katika hukumu peke yake. ´Aqiydah yake ni yenye kuangazwa zaidi kwa Salafiyyah, lakini Imaam Maalik amepatia pale aliposema:

“Hakuna yeyote katika sisi isipokuwa ni mwenye kurudi na kurudiwa isipokuwa mtu mwenye kaburi hili.”

kisha akaashiria kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Anayo baadhi ya mitazamo ambayo inaenda kinyume na mfumo wa Salaf. Lakini yanafunikwa na ´Aqiydah yake kwa kiasi kikubwa ni yenye kuafikiana na ya Salaf. Moja katika makosa yake ninayokumbuka hivi sasa ni kwamba anajuzisha kufanya Tawassul kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Dalili yake ni Hadiyth ya yule bwana kipofu inayotambulika na imetangaa kati ya wanafunzi hii leo na kwamba haijulishi isipokuwa kufanya Tawassul kwa du´aa na uombezi wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kwa hiyo elimu yake inatakiwa kusomwa katika vitabu vyote. Wanafaidika katika mambo mengi ambayo baadhi ya wanachuoni wanayapuuza sembuse wanafunzi. Lakini ayasome kwa kuambatana na dalili ili asije kutumbukia kwenye kosa kama alivyotambukia yeye, sisi na wengine wote wanaosoma elimu wanaweza kutumbukia. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee ndiye ambaye kakingwa na kutumbukia katika makosa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (20 B)
  • Imechapishwa: 31/05/2020