Swali: Kuna wanaoongelea ´Aqiydah ya Imaam ash-Shawkaaniy na khaswa wanaoongelea hilo mbele ya wanafunzi kwenye chuo kikuu. Wafanyavyo ni sahihi?

Jibu: Kitu gani anaweza kumuongelea Imaam ash-Shawkaaniy au asiyekuwa yeye? Akimuongelea mtu lazima aleta dalili ya kosa lake. Ama kuwaponda tu wanachuoni na wala asibainishe hilo. Lazima athibitishe hilo kwa maneno yake. Haiwezekani akajichukulia maneno ya muktadha yanayonasibishwa kwa wanachuoni. Wanachuoni wana vyeo vyao na nafasi zoa. Na Imaam ash-Shawkaaniy ana nafasi yake kunako elimu na uhakiki. Na kaandika uharamu wa kujenga kwenye makaburi. Na kaandika kitabu katika Tawhiyd, “ad-Durr an-Nadhiyd fiy ´Aqiydat-it-Tawhiyd”. Ni Imaam muheshimiwa.Anasema nini huyu masikini? Huenda huyu anayemuongelea ash-Shawkaaniy ana hasira kwake na si ´Aqiydah yake. Kwa kuwa ash-Shawkaaniy ´Aqiydah yake ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Muhaddithuun. Na huyu ana hasira naye kwa kuwa anamkhalifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tg–1431-11-19.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2020