Aina mbili za wazushi

Ahl-us-Sunnah wanaonelea kujitenga na kila mlinganizi katika Bid´ah. Kuna aina mbili za wazushi:

1- Mzushi wa kawaida. Ametumbukia katika Bid´ah na matokeo yake anaathiriwa na walinganizi wa uzushi. Ni vizuri kuchanganyikana na watu sampuli hii, kuwalingania na kuwatengeneza.

2- Mlinganizi anayelingania katika Bid´ah zake na ni kiongozi katika Bid´ah yake ambaye analingania katika Bid´ah yake na kuwapambia watu Bid´ah yake. Huyu anatakiwa kuepukwa. Isipokuwa tu yule ambaye anajiona kuwa ni mwenye nguvu kwenye hoja kumshinda na ana matumaini ya kumshinda. Katika hali hii ampe changamoto na ajadiliane naye. Kuhusu mtu wa kawaida anatakiwa kujitenga naye, kwa sababu mara nyingi wazushi hubeba silaha ya elimu ya balagha ambayo wanaitumia kwa lengo la kutaka kuwapaka watu mchanga wa machoni. Kwa ajili hiyo ndio maana mtu anatakiwa kujitenga na walinganizi wanaolingania katika Bid´ah zao – watu wanaolingania katika ´Aqiydah yao ya Ashaa´irah, ´Aqiydah yao ya Suufiyyah na kadhalika. Wanapaswa kuwaepuka.

Kuhusu mtu ambaye ana matumaini ya kuwasambaratisha, kuwatokomeza na kuwashinda na kuziraddi Bid´ah zao, basi ni lazima kwake kufanya hivo. Pengine hata jambo hili likawa ni faradhi kwa baadhi ya watu.