Kutokuwa na ubinafsi kumegawanyika aina mbili:

1- Kutokuwa na ubinafsi katika mambo ya kujikurubisha kwa Allaah.

2- Kutokuwa na ubinafsi katika mambo ya kidunia.

Kutokuwa na ubinafsi katika mambo ya kujikurubisha kwa Allaah ni jambo limechukizwa kwa kuwa linaenda kinyume na yale tuliyoamrishwa katika kushindana katika mambo ya kheri na kukimbilia katika mambo ya ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) Amesema:

سَابِقُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ

“Kimbilieni katika maghfirah ya Mola wenu.” (57:21)

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ

“Kimbilieni msamaha kutoka kwa Mola wenu na Pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa.” (03:133)

Muislamu anatakiwa kukimbilia na kushindana katika kila mlango miongoni mwa milango ya kheri na amshinde ndugu yake. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ

“Na katika hayo basi washindane wanaoshindana [kufanya mema].” (83:26)

Kutokuwa na ubinafsi katika mambo ya kidunia, bi maana katika chakula, mavazi, kipando, kutangulia mbele katika kikao na mfano wa hayo, haya ni mambo yaliyopendekezwa mtu akawa hana ubinafsi kwa ndugu yake katika mambo ya kidunia. Allaah (´Azza wa Jall) Amesema Akiwasifu waumini maalum:

وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“… na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wana ufukara. Na yeyote yule anayeepushwa na uchoyo wa nafsi yake – basi hao ndio wenye kufaulu.” (59:09)

Aayah imefahamisha juu ya kwamba kutokuwa na ubinafsi katika mambo ya kidunia ni miongoni mwa sifa za waumini. Hii ni dalili inaonyesha mapendekezo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 222-223
  • Imechapishwa: 14/05/2020