3513- Qutaybah ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan adh-Dhwuba´iy ametuhadithia, kutoka kwa Kahmas bin al-Hasan, kutoka kwa ´Abdullaah bin Buraydah, kutoka kwa ´Aaishah aliyesema:

“Ee Mtume wa Allaah! Nisemeje endapo nitajua usiku miongoni mwa nyusiku kwamba ndio usiku wa Qadar?” Akasema: “Sema:

اللَّهُمَّ إِنَّكَ عُفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي

“Ee Allaah! Hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe na unapenda kusamehe. Hivyo basi, nisamehe.”[1]

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3513).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Iysaa Muhammad bin ´Iysaa at-Tirmidhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jaami´ (3515)
  • Imechapishwa: 14/05/2020