Unasema katika barua yako:

“Nilifurahishwa na kichwa cha khabari hichi chenye kuvutia ambacho kilinifanya kutaka kusoma kitabu chote. Mwanzoni nilifikiri kuwa ni maudhui yenye faida kuhusiana na kulingania katika Tawhiyd na mifumo ya Da´wah. Nilipofika katika mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa.”

1- Allaah anajua fika ya kwamba sikusudii kuvunja heshima ya yeyote, si Hasan al-Bannaa wala mtu mwingine. Najua kuwa haki zitachukuliwa siku ya Qiyaamah kwa matendo mema na mabaya.

2- Unajua kuwa kutaja kasoro za mtu inajuzu ikiwa kuna faida ya kufanya hivo. Ni miongoni mwa usengenyi unaofaa. Dalili ya hilo ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia Faatwimah bint Qays wakati alipokuja na kumuomba ushauri (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wa kuolewa na nani. Akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ama Mu´aawiyah ni mtu taabani hana mali. Ama Abu Jahm ni mtu anawapiga wanawake. Olewa na Usaamah bin Zayd.”

3- Unajua kuwa Muhaddithuun wamezungumzia wapokezi katika cheni za wapokezi kwa njia yenye kupelekea mapokezi yao kurudishwa au kudhoofishwa. Wamesema fulani ni mwongo, mzushi, hifdhi dhaifu, anakosea sana, mghafilikaji na kadhalika. Wamefanya hivo kwa kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah, Mtume Wake, waislamu na kuilinda Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kusiingizwe ndani yake yasiyokuwemo.

4- Wewe mwenyewe umesema katika kitabu chako:

“Inatakiwa kuchunguza hali za wapokezi na kutafiti nafasi zao katika Hadiyth na upeo wao. Wanachuoni wamezungumza juu yao kwa ajili ya kutoa nasaha kwa Ummah kwa vile wamejivisha jukumu la kufikisha sehemu ya dini ilio na hukumu. Wamekhusisha aina hii [kuwa inajuzu] kwa makatazo ya kijumla ya kusengenya kutokana na manufaa yanayopatikana kwa Ummah mzima.”[1]

Hili ni sahihi kabisa.

5- Jifikirie ni kitu gani kilichonifanya mimi kumraddi mtu huyu ambaye amekufa pindi nilipokuwa bado mdogo. Hakumwaga damu yangu. Hakuvunja heshima yangu. Hakuchukua mali yangu. Ni kitu gani kimechonifanya mimi kutahadharisha juu yake ilihali hakunifanya lolote? Ikiwa nimemsema vibaya bila ya yeye kunifanya chochote na bila ya maslahi ya kidini yanayopatikana, basi mimi nimemdhulumu na hivyo Allaah atachukua haki yangu na kumpa yeye.

6- Leo tumetahiniwa na mifumo mbalimbali ya ki-Da´wah. Imetoka nje ya nchi yetu. Inachukulia wepesi shirki kubwa. Wanachukulia wepesi Tawhiyd na Bid´ah. Miongoni mwa mifumo hiyo muhimu na ilioenea sana kwa kueneza ufisadi na uharibifu mkubwa ni mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Wanasafisha akili za vijana wanaolelewa humo. Wanawafanya kuwa watu wa mapinduzi, Takfiyriyyuun, maigaidi na Khawaarij. Kuna dalili nyingi juu ya hilo. Katika dalili zilizo muhimu zaidi ni kukubali kwa wahalifu waliolipua ´Ulayyaa ar-Riyaadh kama ´Abdul-´Aziyz al-Mu´thim na marafiki zake. Hili ndio limelonifanya kuandika juu yake na chama chake kabla ya kutokea malipuzi haya.

7- Umeandika:

“Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa. Unamshambulia na kufasiri maneno yake kimakosa.”

a) Lau ungelisoma kitabu chote kwa inswafu, basi ungelijua kuwa nilichofanya ni mimi kubainisha tu jinsi mfumo huu na muasisi wake anavotumbukia kwenye makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ya Kiislamu na ´Aqiydah ya Salaf. Yeye ndiye ambaye amesema, na kaka yake amekubali na kujifakharisha kwa hilo na ni jambo limeenea katika vitabu vya pote lake:

“Ee Allaah! Sema na uache uwepo na yale yaliyomo. Ikiwa umeelewa, basi utaona kuwa hakuna aliyepo isipokuwa Allaah, si maalum wala jumla.”[2]

Ikiwa wewe unaonelea kuwa nimeyafasiri maneno yake kimakosa, ninakuomba unifasirie wewe maneno yake haya kwa njia inayokubalika Kishari´ah na kiakili pasi na kuingia kwenye Wahdat-ul-Wujuud.

b) Vilevile yeye ndiye alikuwa akiimba:

“Ee Allaah, swalia nuru (yaani Mtume) Ulioifanya kuja kwa walimwengu na inayoangazia kwa jua na mwezi. Mpenzi huyu (yaani Mtume) amehudhuria pamoja na wapenzi wake na amemsamehe kila mmoja kwa yaliyopitika.”

Nifasirie matamshi haya kwa njia ambayo haina shirki kubwa pindi anaposema:

“Mpenzi huyu (yaani Mtume) amehudhuria pamoja na wapenzi wake na amemsamehe kila mmoja kwa yaliyopitika.”?

Unaweza kunifasiria matamshi haya kwa njia isiyokuwa ya kumzulia uongo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na uongo wa Suufiyyah pindi wanaposema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anahudhuria sherehe zao za kizushi wakati wanaposherehekea mazazi ya Mtume?

c) Unaweza kunifasiria kumsifu kwake al-Marghaniy ambaye alikuwa anajulikana kwa Wahdat-ul-Wujuud kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini pasi na kuridhia Wahdat-ul-Wujuud na kuwasifu wenye nayo?

d) Unaweza kunifasiria maneno yake “Kati yetu sisi na mayahudi hakuna uadui wa kidini” kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini isiyokuwa ya kuwapaka mafuta mayahudi na manaswara na kumsemea uongo Allaah, Mtume Wake na Uislamu?

e) Unaweza kunifasiria muhadhara wake kwenye kaburi la Zaynab katika mnasaba wa kusherehekea mwaka mpya wa Kiislamu bila ya kutaja shirki na kukataza hilo pamoja na kwamba anaona jinsi watu wanavolizunguka kaburi na kuliomba kitu ambacho hakiombwi isipokuwa kutoka kwa Allaah pekee? Nifasirie muhadhara huo kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini pasi na kuridhia shirki kubwa na kujihalalishia hayo kwa nafsi yake na mfumo wake?

f) Unaweza kunifasiria kwenda kwake katika kaburi la ad-Dasuuqiy na Sanjar kwa umbali wa kilomita 40 kwenda na kurudi kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini bila ya matembezi ya kishirki au ya kizushi?

g) Unaweza kunifasiria njama zake za kufanya Ahl-us-Sunnah na Raafidhwah wakaribiane kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini pasi na ujinga wa Bid´ah na upotevu wa Raafidhwah, au kuchukulia wepesi upotevu wao, na kwa hivyo kuitoa fidia ´Aqiydah ya Kiislamu kwa ajili ya kuwaridhisha Raafidhwah?

h) Unaweza kunifasiria kujigonga kwake anaposema kuwa Da´wah yake ni Salafiyyah, njia yake ni ya ki-Sunnah na uhakika wake ni Suufiyyah? Je, ni jambo linalowezekana Suufiyyah ikawa pamoja na Salafiyyah na Suufiyyah na Sunnah? Ni kama mfano wa kukutanisha moto na maji.

i) Unaweza kunifasiria nguzo kumi za kiapo chake cha utiifu umejengeka juu ya kitu gani kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini pasi na kuleta Da´wah ilio na Shari´ah mpya?

j) Unaweza kunifasiria maneno yake anaposema kuwa madhehebu ya Salaf wote katika sifa ni kumtegemezea Allaah maana yake kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini kama sio ujinga juu ya madhehebu ya Salaf katika sifa, au kuwasemea uongo, kwa vile tunajua kuwa Salaf wanaamini maana pasi na kujua namna yake?

Ukinifasiria maneno haya kwa tafsiri isiyopingana na Shari´ah na lugha, basi nastahiki maneno yako pale ulipoandika kuwa nimefasiri maneno yake kimakosa. Ukishindwa kufanya hivo, basi itabainika kuwa umenizulia uongo. Utambue kuwa sintokuomba haki yangu isipokuwa mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah. Hata hivyo nataka tumuweke Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz, Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh, Shaykh Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan, Shaykh ´Abdullaah al-Ghudayyaan na Shaykh Swaalih al-Atram kati yako wewe na mimi ili wasome mlango wa tisa kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho. Wakiona kuwa nimefasiri maneno ya al-Bannaa kimakosa, basi wanihukumu. Na wakiona kuwa mtu ambaye amesema hivo ndio amenidhulumu na kunisemea uongo, basi wamhukumu.

[1] “Akhbaar-ul-Aahaad”, uk. 30

[2] Hasan al-Bannaa bi Aqlaam Talaamiydhih wa Mu´aaswiriyh, uk. 70-71.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 6-13
  • Imechapishwa: 05/07/2020