Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kumwambia myahudi na mnaswara kuwa ni makafiri?

JIbu: Inajuzu kwa muislamu kumwambia myahudi au mnaswara kuwa ni kafiri. Allaah amewasifu katika Qur-aan kwa wasifu huu. Hili ni jambo linalojulikana kwa yule aliyeizingatia Qur-aan. Miongoni mwa hayo ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ

“Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika Moto wa Jahannam – ni wenye kudumu humo milele – hao ndio waovu wa viumbe.” (98:05)

Ahl-ul-Kitaab ni mayahudi na manaswara.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/94)
  • Imechapishwa: 24/08/2020