as-Swaabuuniy amekufa katikati ya karne ya 500. Hata baada yake waliishi maimamu wa Uislamu na wanachuoni kama wanachuoni wa Jerusalemu (Maqaadisah), Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, adh-Dhahabiy, Ibn Kathiyr na wengine wengi ambao waliitumikia Sunnah na kuopandisha bendera yake. Baada yao akaja Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na wanafunzi zake. Kundi hili halitokatika kamwe kwa mujibu wa maneno ya mkweli na mwaminifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakutoacha siku zote kuendelea kuwepo kwa kundi katika Ummah wangu lenye kunusuriwa katika haki. Halitodhuriwa na wale wenye kuwapinga na kwenda kinyume nao mpaka amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ije.”

Mtu ana mfumo gani ikiwa anamchukia Ibn Taymiyyah na Ibn ´Abdil-Wahhaab (Rahimahumaa Allaah)?

Mtu ana mfumo gani ikiwa anamchukia Ibn Baaz, al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn na watu mfano wao? Ni katika Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal bila ya shaka. Unaweza kuona jinsi makundi yanaacha kuwatakia rahmah. Wanawachukia na kwenda kinyume nao na mfumo wao. Kituo chao ni kituo cha Ahl-ul-Bid´ah.

Tunawapenda wanachuoni hawa kwa sababu wamehifadhi na kufikisha Sunnah na ´Aqiydah. Wameipigania. Allaah Awarahamu! Tunasimama katika upande wao na tunawapenda. Kuwachukia ni alama ya Ahl-ul-Bid´ah. Kadhalika watu waliokuja baada yao ambao wana mfumo wao. Ni Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal ndio wanawachukia.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 349
  • Imechapishwa: 23/04/2015