as-Swaabuuniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ahl-us-Sunnah wanawapenda maimamu wa Shari´ah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanachuoni wa Ummah huu.”

Ni katika zawadi ya Allaah. Yule mwenye kuwachukia Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wale wenye kuwaiga kati na kati au wanachuoni pasina kujali wakati, Amekataliwa na Allaah. Kuwachukia wanachuoni na watu wema ni alama ya kukataliwa na ubaya. Watu hawa ni wajuzi zaidi juu ya Allaah, Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuzitendea kazi. Kwa nini unawachukia? Unawachukia kwa sababu tu Allaah Amekukataa na kwa kuwa Hakutakii kheri midhali hutubii kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 342
  • Imechapishwa: 23/04/2015