Swali: Je, inafaa kumwita mlinganizi wa upotevu kwamba ni ´shaytwaan`?

Jibu: Ndio, ni miongoni mwa mashaytwaan wa kibinadamu. Mashaytwaan wa kibinadamu khatari yao ni kubwa zaidi kuliko mashaytwaan wa kijini. Kwa sababu Allaah ameanza kuwataja wao kwanza na akasema:

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا

“Vivyo hivo tumemfanyia kila Nabii maadui mashaytwaan wa kiwatu na kijini – wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba  – kwa udanganyifu.”[1]

Ameanza kuwataja wao kwanza. Haya ni kwa sababu khatari yao ni kubwa zaidi.

[1] 06:112

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (99) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86-10-07-1440%D9%87%D9%80_0.mp3
  • Imechapishwa: 02/08/2020