Swali: Ni ipi faida ya kuchukua ahadi kutoka mgongo wa baba yao Aadam?

Jibu: Makusudio ni kwamba ahadi ilichukuliwa kupitia Aadam, na si kwa mtu mmojammoja. Ahadi ilichukuliwa kupitia Aadam peke yake. Kuhusu mtu mmojammoja ahadi inachukuliwa kwake kupitia Mitume wanaomjia.

 Swali: Nini makusudio ya:

أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا

“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia!”[1]?

Jibu: Hii ilikuwa katika migongo yao; ahadi haichukuliwi kutoka kwao isipokuwa baada ya kujiwa na Mitume.

[1] 07:172

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31369/ما-الحكمة-من-اخذ-العهد-من-ظهور-بني-ادم
  • Imechapishwa: 23/10/2025