Adhkaar kwa utaratibu ipasavyo baada ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Adhkaar kwa utaratibu ipasavyo (الترتيل) baada ya swalah za faradhi?

Jibu: Kusoma namna hiyo inakuwa Qur-aan peke yake:

وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا

“… soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu na utungo.”[1]

Kitu kingine hakitakiwi kufananishwa na Qur-aan.

[1] 73:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 25/05/2023