Adhanaa ya kwanza Fajr nje ya Ramadhaan

Swali: Je, adhaana ya kwanza ya al-Fajr kinyume na Ramadhaan imethibiti na ni ipi dalili ya hilo?

Jibu: Sikumbuki kitu kwa sasa isipokuwa katika Ramadhaan tu. Adhaana ya kwanza nakumbuka katika Ramadhaan tu ambapo Bilaal alikuwa akiadhini usiku kisha baada yake anaadhini Ibn Umm Maqtuum. Sikumbuki juu ya hili kitu. Ingawa wanachuoni wametumia Qiyaas miezi mingine nje ya Ramadhaan. Hili ndio ninalokumbuka. Sikumbuki kitu maalum juu ya miezi mingine. Kisha wakasema maana ya adhaana ya kwanza ni ili iwazindue watu – kama ilivyo katika Hadiyth ya Bilaal. Mwenye kulala anazinduka na kujua kuwa al-Fajr iko karibu ili aweze kujiandaa. Ama andiko la wazi kabisa kuhusu adhaana ya kwanza nje ya Ramadhaan sikumbuki kitu. Linahitajia kutiliwa umuhimu. Huenda [dalili ipo] lakini sikumbuki kitu kwa sasa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6898
  • Imechapishwa: 03/12/2014