Swali: Mwenye kutawadha akaumia mkono wake au mguu wake mpaka akatokwa na damu. Je, Wudhuu wake ni wenye kuvunjika?

Jibu: Haidhuru. Damu ndogo haivunji Wudhuu. Tofauti iliyopo ni kuhusu damu nyingi ikitoka inavunja Wudhuu au hapana. Ama kuhusu damu ndogo inayotoka mkononi au mguuni hii hakuna tofauti kwamba haivunji Wudhuu na haidhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6898
  • Imechapishwa: 03/12/2014