767- Ahmad ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-Qaasim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aaishah ambaye amesimulia kwamba alipata ada yake ya mwezi punde tu kabla ya kufika Makkah ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

“Fanya kila anachofanya mwenye kuhiji.”

Ahmad amesema: Mara nyingine Sufyaan alisimulia Hadiyth namna hii:

“Fanya kila anachofanya mwenye kuhiji isipokuwa tu usitufu kwenye Nyumba.”

768- Ahmad ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Muusa bin ´Uqbah, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Ibn ´Umar ambaye amesema:

“Anatakiwa kufanya kila anachofanya mwenye kuhiji isipokuwa tu asitufu kwenye Nyumba na kutembea kati ya Swafaa na Marwah.”

769- Ahmad ametuhadithia: ´Abdur-Razzaaq ametuhadithia, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa az-Zuhriy ambaye amesema:

“Mwanamke akipata ada yake ya mwezi baada ya kutufu kwenye Nyumba, basi atembee kati ya Swafaa na Marwah wakati wa hedhi yake.”

770- Ahmad ametuhadithia: Rawh ametuhadithia: Ash´ath ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan aliyesema ikiwa mwanamke atapata ada yake ya mwezi baada ya kutufu katika Nyumba lakini kabla ya kuswali Rak´ah mbili nyuma ya maeneo ya Ibraahiym na kutembela kati ya Swafaa na Marwah:

“Anatakiwa kutembea. Hizo Rak´ah mbili ataziswali baada ya kutwahirika.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 162
  • Imechapishwa: 26/03/2021