Acha kusoma al-Faatihah na mfuate imamu

Swali: Ikiwa imamu amerukuu kisha mtu akataka kumaliza kusoma al-Faatihah, lakini imamu akainuka kabla ya yeye kumaliza kusoma al-Faatihah?

Jibu: Aikate na arukuu pamoja naye.

Swali: Lakini ikiwa imamu ameinuka kabla hajamaliza kuisoma?

Jibu: Ainame na amuwahi. Ni mwenye kupewa udhuru – Allaah akitaka. Arukuu na amuwahi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25227/ما-الحكم-اذا-ركع-الامام-واكمل-الماموم-قراءة-الفاتحة-فرفع-الامام
  • Imechapishwa: 20/02/2025