Asiyekuwa na kitu hawezi pia kutoa chochote. Tunamwambia ´Abdullaah as-Sabt aje na mwanafunzi mmoja bingwa katika wanafunzi zake. Na mwambie mwalimu wako ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq aje na mwanafunzi mmoja bingwa. Tunampa changamoto. Wakisema kuwa ash-Shaayijiy ni bingwa na amesema hili na lile kwa ´Abdur-Rahmaan… Kisha isitoshe ash-Shaayijiy ni mpumbavu. Ndio, ni sahihi kwamba ni mpumbavu. Amewasemea uongo Ahl-us-Sunnah katika kitabu chake. Wanafunzi zako, ´Abdur-Rahmaan, ni wapumbavu kama mfano wa ash-Shaayijiy? Umepotea na kukhasirika ikiwa ni wapumbavu kama ash-Shaayijiy, na Allaah ndiye Anayetakwa msaada.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbil.net/sounds.php?sound_id=28
  • Imechapishwa: 22/04/2015