Kipambanuzi kinachotilia nguvu ndani ya Qur-aan ni maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.”[1]

Ibn ´Abbaas amesema:

“Sio ule ukafiri unaomtoa mtu nje ya dini.”[2]

´Atwaa´ bin Abiy Rabaah amesema:

“Ni ukafiri mdogo.”

Hapa imetubainikia kuwa kitendo hicho si chenye kumtoa mtu nje ya Uislamu, ikiwa na maana kwamba dini ni yenye kubaki kama ilivyo. Hata kama ataichanganya na madhambi, haina maana nyingine isipokuwa kuwa na sifa za makafiri, kama ilivyo katika shirki. Kwa sababu ni katika sifa za makafiri kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah. Hukumsikia pale aliposema:

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

“Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.”[3]?

Kwa mujibu wa wafasiri maana ya Aayah ni kwamba muislamu anayehukumu kwa yale ambayo hakuteremsha Allaah, kwa hukumu hiyo amefanana na watu waliokuwa wakihukumu kwa hukumu kabla ya kuja Uislamu, kwa sababu hivo ndivo walivyokuwa wanafanya.

[1] 5:44

[2] al-Haakim (2/313) kupitia Twaawuus, kutoka kwa Ibn Mas´uud. Wote wawili yeye na adh-Dhahabiy wameisahihisha.

[3] 5:50

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy