Kuhusu yaliyokuja katika Sunnah ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kikubwa ninachokikhofia juu ya ummah wangu ni shirki ndogo.”

Hapa amekufafanulia kuwa kuna aina nyingine ya shirki ambayo haimfanyi mwenye nayo ni mwenye kumshirikisha Allaah. Mionogni mwa aina zake ni maneno yake ´Abdullaah:

“Ribaa ni sampuli sitini na kitu – vivyo hivyo kuhusu shirki.”[1]

Hapa amekukhabarisha kuwa kuna madhambi mengi yaliyobeba jina hilo pasi na kuwa ile shirki yenye maana ya kuwaabudu wengine wasiokuwa Allaah – Allaah ametakasika kutokana na hilo kutakasika kukubwa! Kwa mtazamo wangu mimi sioni kuwa madhambi haya yanaweza kufasiriwa kwa njia nyingine isipokuwa tabia za washirikina, majina yao, desturi zao, matamshi yao, hukumu zao na kadhalika.

[1] Ameipokea al-Bazzaar kupitia kwa Ibn Mas´uud, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wapokezi wake ni wapokezi Swahiyh, ndivo alivosema al-Mundhiriy na al-Haythaymiy. Kwa Ibn Maajah hakukutajwa shirki. Cheni ya wapokezi wake pia ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy