Hayo pia ndio yanayoweza kusemwa kuhusu maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mambo matatu ni katika mambo kabla ya kuja Uislamu: kutukaniana nasaba, kuomboleza na alama ya nyota.”[1]

Vivyo hivyo kuhusu Hadiyth aliyoipokea Jariyr na Abul-Bakhtariy at-Twaa-iy:

“Mambo matatu ni katika mambo kabla ya kuja Uislamu: kuomboleza, kutengeneza chakula na mwanamke kulala kwa wafiwa wengine.”[2]

Vivyo hivyo Hadiyth:

“Alama za mnafiki ni tatu; anapozungumza husema uwongo, anapoahidi huvunja ahadi na anapoaminiwa hukhaini.”[3]

´Abdullaah amesema:

“Nyimbo zinaotesha unafiki moyoni.”[4]

Muda wa kuwa mwenye kufanya madhambi haya anamwamini Allaah na ujumbe Wake na anatekeleza faradhi Zake, hazifahamishi kabisa kuwa anakuwa katika kile kipindi cha kishirikina kabla ya kuja Uislamu au kwamba anakuwa kafiri au mnafiki. Lakini maana yake zinabainisha kuwa ana matendo kama ya makafiri na yamekatazwa ndani ya Qur-aan na Sunnah ili waislamu waweze kuyaepuka na kujitenga nayo mbali na hivyo wasijifananishe na chochote katika tabia wala Shari´zao. Kumepokelewa katika baadhi ya Hadiyth:

“Nyeusi ni katika rangi za makafiri.”[5]

Je, hivi kweli mtu anaweza kutuhumiwa ukafiri kwa sababu tu amezitia nywele zake rangi nyeusi? Kadhalika Hadiyth inayosema kuwa mwanamke anyejitia manukato kisha akawapitia mkusanyiko watu wataohisi ile harufu yake, ya kwamba ni mzinzi[6]. Je, hii ina maana ya mzinzi ambaye anapaswa kuadhibiwa? Vilevile kuhusu Hadiyth isemayo:

“Watukanaji wawili ni mashaytwaan wawili ambao wanatiana kwenye batili na kukadhibishana.”[7]

Je, kuna mtu anayefikiria kuwa alikusudia mashaytwaan ambao ni katika wana wa Ibliys? Hakika mambo si vyenginevyo ni kama nilivyokufunza, kwamba inahusiana na matendo, tabia na sifa.

[1] Hadiyth ni Swahiyh ambayo ameipokea al-Bukhaariy katika ”at-Taariykh al-Kabiyr” na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1/105/2) kupitia kwa Junaadah bin Maalik, al-Bazzaar kupitia kwa ´Amr bin ´Awf, Ibn Jariyr kupitia kwa Abu Hurayrah na Anas bin Maalik, na kupitia kwake Abu Ya´laa kutoka kwa Anas kwa ufupi na kwa cheni ya wapokezi yenye nguvu, kama ilivyokuja katika ”Fath-ul-Baariy” (12/37). Kwa al-Bukhaariy imepokelewa kama maneno ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

[2] Hadiyth ya Jariyr bin ´Abdillaah al-Bajaliy ameipokea Ibn Maajah (1612) kupitia kwa Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid, kutoka kwa Qays bin Abiy Haazim, kutoka kwa Jariyr ambaye amesema:

“Tulikuwa tunaona kukusanyika kwa wafiwa na kutengeneza chakula baada ya mazishi ni katika maombolezo.”

Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

Kuhusu Hadiyth ya Abul-Bakhtariy – ambaye jina lake anaitwa Sa´iyd bin Fayruuz na ambaye alikuwa katika wanafunzi wa Swahabah na mtu mwaminifu – sijaipata.

[3] al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

[4] Abu Daawuud (4927) kupitia kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu.

[5] at-Twabaaraaniy na al-Haakim. Hadiyth ni dhaifu. adh-Dhahabiy amesema:

“Ni Hadiyth munkari.”

[6] Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh”, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Haakim katika ”al-Mustadrak” kupitia kwa Abu Muusa al-Ash´ariy, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Mwanamke yeyote ambaye atajitia manukato na akapita kando na watu ili wahisi harufu yake, basi ni mzinifu.”

Abu Daawuud na at-Tirmidhiy wamepokea mfano wake na wameisahihisha.

[7] Hadiyth ni Swahiyh na ameipokea al-Bukhaariy katika ”al-Adab al-Mufrad”, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na Ahmad kupitia kwa ´Iyaadh bin Himaar (Radhiya Allaahu ´anh). Imetajwa katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´ as-Swaghiyr” (6572).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 90-93
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy