Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Uhakika wa mambo wanachotaka kusema ni kwamba utambuzi wa kumjua Allaah (´Azza wa Jall), majina na sifa Zake hautafutwi kutoka ndani ya Qur-aan, Sunnah na kwa Salaf. Badala yake kila mmoja afikirie mwenyewe; zile sifa ambazo mtu kwa kutumia akili yake anaona zinamstahikia Allaah basi amthibitishie nazo, ni mamoja zipo ndani ya Qur-aan na Sunnah au hazipo. Na zile sifa ambazo mtu kwa kutumia akili yake anaona kuwa hazimstahikii Allaah basi asimthibitishie nazo.

MAELEZO

Kwa mujibu wa maneno ya watu hawa ni kwamba yanapelekea kuwaambia watu wasichukue ´Aqiydah kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah, kwa sababu ndani yake hakuna ´Aqiydah sahihi na badala yake waichukue kutoka katika maneno, I´tiqaad na fikira za watu. Kwani hayo ndio sahihi. Yale yanayofahamishwa na akili na fikira zao kuhusu Allaah ndio haki na wala wasiangalie ndani ya Qur-aan, Sunnah wala maneno ya Salaf. Kwa sababu hao hawana utambuzi wa mambo hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 144
  • Imechapishwa: 02/09/2024