98. Yako matendo ambayo ni ukafiri

Maneno ya mtunzi yasifahamike namna hii moja kwa moja kwa njia ya kuachia. Yako matendo yanayomtia ukafirini mwenye nayo. Kama mfano kuacha swalah. Yule mwenye kuacha swalah kwa makusudi anakufuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi ilioko baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”[1]

“Baina ya mja na kufuru na shirki ni kuacha swalah.”[2]

Kuacha swalah kunamtia mtu ukafirini. Maneno ya mtunzi:

“Hakuna yeyote katika watu wa Qiblah anayekufuru kwa dhambi.”

Bi maana waislamu wapwekeshaji wanaoswali kuielekea Ka´bah. Ka´bah ndio Qiblah cha waislamu wote.

[1] at-Tirmidhiy (2621), an-Nasaa’iy (463) na Ibn Maajah (1079). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[2] Muslim (82).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 75
  • Imechapishwa: 26/08/2021