Swali 98: Je, kufanya maandamano ni moja katika njia za ulinganizi kwa ajili ya kutatua matatizo ya ummah wa Kiislamu?

Jibu: Dini yetu sio dini ya fujo. Dini yetu ni dini ya nidhamu, dini ya utaratibu na dini ya utulivu. Maandamano sio katika matendo ya waislamu. Hapo kabla Uislamu hakuwa unayatambua. Uislamu ni dini ya rehema, si dini ya vurugu, tashwishi wala dini ya kuchochea fitina.

Haki zinaweza kufikiwa kwa njia zingine na njia zilizowekwa katika Shari´ah. Maandamano haya yanazalisha mitihani mingi, umwagikaji wa damu na kuharibu mali. Kwa hivyo mambo haya hayajuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 231-232
  • Imechapishwa: 07/08/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy