Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Pale walipokanusha sifa na wakati huohuo maandiko yakalazimu kuwa na maana, ndipo wakabaki hali ya kuwa ni wenye kusita kati ya kuamini tamko na kuegemeza maana, kitu ambacho wanaita kuwa ndio mfumo wa Salaf, na kuligeuza tamko kwenda katika maana nyingine, kitu ambacho wanaita kuwa ndio mfumo wa wale waliokuja nyuma.

MAELEZO

Wakati walipokanusha sifa za Allaah, licha ya kuwa zimethibitishwa na Qur-aan na Sunnah katika maandiko mengi na hawawezi kuzikataa, wakagawanyika mafungu mawili:

1 – Baadhi wakazipindisha maana na kuzikengeusha. Hawa wanaitwa Mu´attwilah.

2 – Wengine wakanyamaza na kutegemeza maana yake kwa Allaah. Hawa wanaitwa Mufawwidhwah. Wanasema kuwa hawayafasiri maandiko na kwamba wanategemeza tafsiri yake kwa Allaah. Aidha wanaongeza kuzindua kuwa maandiko hayafahamishi sifa. Wanasema kuwa hawajui maana ya maandiko na wanawanasibishia mwenendo huo Salaf. Wamenasibisha ugonjwa wao kwa Salaf na wakarusha mawe katika nyumba za vioo. Wao ndio Mufawwidhwah, si Salaf.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 07/08/2024