Hoja tata nyingine ya tatu ni kwamba tukiyathibitisha maandiko haya ilihali yanapatikana kwa viumbe, kama vile kusikia, kuona, maneno, uwezo, mkono na uso, tutakuwa tumemfananisha Allaah na viumbe. Hivo ndivo wanafikiria. Wanaona wasithibitishe sifa hizi ili wasimfananishe Allaah na viumbe Wake, hivo ndivo wanavosema.
Hoja tata hii inaraddiwa kwamba njia ya kuwa sifa za viumbe zinalingana na uumbaji wao. Allaah amejisifu Mwenyewe kwa sifa Zake – na Yeye ni mjuzi zaidi wa nafsi Yake. Hiyo ikafahamisha kuwa sifa za Allaah si kama sifa za viumbe. Hazifanani hata kama zitashirikiana upande wa jina. Hazishirikiani upande wa uhakika na namna. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anazo sifa zinazolingana Naye na hakuna anayejua namna Yake isipokuwa Yeye tu. Viumbe pia wanazo sifa zinazolingana nao. Kusikia kwao si kama kusikia kwa Allaah, kuona kwao si kama kuona kwa Allaah, ujuzi wao si kama ujuzi wa Allaah, uwezo wao si kama uwezo wa Allaah, mikono yao si kama mkono wa Allaah, nyuso zao si kama uso wa Allaah na kadhalika. Ameanza kusema (Ta´ala):
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “[1]
Baada ya hapo akasema:
وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
“… Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[2]
Amejithibitishia Mwenyewe kusikia na kuona, licha ya kuwa sifa hizo mbili zinapatikana kwa viumbe:
إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا
“Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na tone la manii iliyochanganyika ili Tumjaribu, hivyo tukamjaalia mwenye kusikia na kuona.”[3]
Mtu anasikia na kuona – na Allaah anasikia na kuona:
وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
“… Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[4]
Upande mmoja amejibitishia Mwenyewe kusikia na kuona. Upande mwingine Akakanusha kufanana:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “
Hivyo ikajulisha kuwa kusikia kwao si kama kusikia kwa Allaah na kuona kwao si kama kuona kwa Allaah. Hii ndio kanuni inayotumika katika sifa zote za Allaah (´Azza wa Jall). Sifa za Allaah zimethibiti kwa Allaah kwa njia isiyofanana na sifa za viumbe. Endapo Allaah angeliwaongoza katika haya basi wangelishusha pumzi kutoka katika tabu hii na wakashika njia ya Salaf ambayo ni kuzithibitisha sifa za Allaah kama zilivyokuja na kihakika na wakazikanushia mashabihisho na mafanano.
[1] 42:11
[2] 42:11
[3] 76:2
[4] 42:11
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 81-82
- Imechapishwa: 07/08/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 81-82
Imechapishwa: 07/08/2024
https://firqatunnajia.com/47-watu-wanasikia-na-kuona-allaah-anasikia-na-kuona/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)