Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kwa sababu hawaoni kuwa maandiko yanafahamisha sifa na wanaijengea nadharia yao hoja tata ambazo wanashirikiana na ndugu zao katika makafiri.
MAELEZO
Wamepotea kutokana na hoja tata hii. Hoja tata ya kwanza ni kwamba wamefikiria kuwa Salaf hawajui maana ya maandiko haya.
Hoja tata nyingine wamedhani kuwa Allaah hana sifa, kwamba maandiko haya yanafahamisha juu ya sifa za Allaah na kwamba hazitakiwi kufahamika juu ya udhahiri wake. Kwa ajili hiyo zinatakiwa kufasiriwa na kugeuzwa kutoka katika udhahiri wake. Hii ndio sababu ya upotofu; hawaamini sifa za Allaah. Ilipokuwa kwamba hawaziamini sifa za Allaah na udhahiri wa maandiko haya ni kuwa yanathibitisha sifa ndipo wakajaribu kuyageuza kutoka katika udhahiri wake na hivyo yapate kuafikiana na matamanio yao. Hiyo ndio mbinu ya kila mpotofu ulimwenguni.
Sababu ya upotofu wao ni ukanushaji. Wamemkanushia Allaah sifa kwa sababu hawaamini kuwa Allaah yuko na sifa. Wanaona kuwa Allaah ni dhati tu isiyokuwa na sifa. Nini walichofanya ilipokuwa maandiko yako wazi katika kumthibitishia Allaah sifa? Kwa vile hawawezi kuyakadhibisha maandiko, ndipo wakaamua kuyapindisha maana. Wakakengeusha maana na kuyageuza kutoka mahali pake stahiki. Matokeo yake wakakimbia kitu ambacho wameona kuwa ni upotofu na wakatumbukia katika upotofu mkubwa zaidi.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 80-81
- Imechapishwa: 07/08/2024
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kwa sababu hawaoni kuwa maandiko yanafahamisha sifa na wanaijengea nadharia yao hoja tata ambazo wanashirikiana na ndugu zao katika makafiri.
MAELEZO
Wamepotea kutokana na hoja tata hii. Hoja tata ya kwanza ni kwamba wamefikiria kuwa Salaf hawajui maana ya maandiko haya.
Hoja tata nyingine wamedhani kuwa Allaah hana sifa, kwamba maandiko haya yanafahamisha juu ya sifa za Allaah na kwamba hazitakiwi kufahamika juu ya udhahiri wake. Kwa ajili hiyo zinatakiwa kufasiriwa na kugeuzwa kutoka katika udhahiri wake. Hii ndio sababu ya upotofu; hawaamini sifa za Allaah. Ilipokuwa kwamba hawaziamini sifa za Allaah na udhahiri wa maandiko haya ni kuwa yanathibitisha sifa ndipo wakajaribu kuyageuza kutoka katika udhahiri wake na hivyo yapate kuafikiana na matamanio yao. Hiyo ndio mbinu ya kila mpotofu ulimwenguni.
Sababu ya upotofu wao ni ukanushaji. Wamemkanushia Allaah sifa kwa sababu hawaamini kuwa Allaah yuko na sifa. Wanaona kuwa Allaah ni dhati tu isiyokuwa na sifa. Nini walichofanya ilipokuwa maandiko yako wazi katika kumthibitishia Allaah sifa? Kwa vile hawawezi kuyakadhibisha maandiko, ndipo wakaamua kuyapindisha maana. Wakakengeusha maana na kuyageuza kutoka mahali pake stahiki. Matokeo yake wakakimbia kitu ambacho wameona kuwa ni upotofu na wakatumbukia katika upotofu mkubwa zaidi.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 80-81
Imechapishwa: 07/08/2024
https://firqatunnajia.com/46-upotofu-mmoja-na-kuingia-upotofu-mbaya-zaidi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)