´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Roho ina mafungamano matano na mwili na hivyo hukumu tofauti:

1- Mafungamano yake tumboni mwa mama.

2- Mafungamano yake inapotoka katika dunia hii.

3- Mafungamano yake wakati wa usingizi. Katika hali hii inakuwa na mafungamano nao kwa njia moja na imetengana nao kwa njia nyingine.

4- Mafungamano yake katika Barzakh. Hata kama inatengana nao haifanyi hivo kikamilifu. Hurudi wakati wa mitihani na inaitikia salamu wakati inaposalimiwa.

5- Mafungamano yake siku ya Qiyaamah. Haya ndio mafungamano yaliyo kamilifu. Hayawezi kulinganishwa na mafungamano yaliyo kabla yake. Katika mafungamano haya mwili haukubali kufa, kusinzia au kuharibiwa na Allaah ndiye anajua zaidi.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa kwa mapokezi mengi zinathibitisha kuwa roho inarudishwa kiwiliwilini wakati wa kuhojiwa. Baadhi wanasema kuwa mwili unahojiwa bila ya roho, jambo ambalo limepingwa na jamhuri. Wengine wakasema kuwa kinachohojiwa ni roho pasi na mwili. Haya yamesemwa pia na Ibn Maysarah na Ibn Hazm. Maoni yote mawili ni ya makosa. Hadiyth Swahiyh zinayarudi na Allaah ndiye anajua zaidi.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 208-209
  • Imechapishwa: 07/12/2016