96. Du´aa ya kuingia kijiji au mjini

  Download

208-

أللّـهُمَّ رَبَّ السَّـمواتِ السّـبْعِ وَما أَظْلَلَـنَ، وَرَبَّ الأَراضيـنَ السّـبْعِ وَما أقْلَلْـنَ، وَرَبَّ الشَّيـاطينِ وَما أَضْلَلْـنَ، وَرَبَّ الرِّياحِ وَما ذَرَيْـنَ، أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَ هذهِ الْقَـرْيَةِ وَخَيْـرَ أَهْلِـها، وَخَيْـرَ مَا فِيهَا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها وَشَـرِّ أَهْلِـها، وَشَـرِّ مَا فِيهَا

“Ee Allaah! Mola wa mbingu saba na kila ambacho hizo mbingu zimekipa kivuli, Mola wa ardhi saba na kila ambacho zimekibeba, Mola wa mashaytwaan na kila walichokipoteza, Mola wa pepo na zilichokibeba. Nakuomba kheri ya kijiji hichi na kheri ya wakazi wake na kheri ya vilivyomo ndani yake. Pia najilinda Kwako na shari ya kijiji hichi, shari ya wakazi wake na shari ya yaliyomo ndani yake.”[1]

[1] al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy  akaafikiana naye (02/100 na Ibn-us-Sunniy (524). Haafidhw ameifanya kuwa nzuri katika  ”Takhriyj-ul-Adhkaar”  (05/154). Ibn Baaz amesema:

”Ameipokea an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi nzuri. Tazama “Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk.370.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 04/05/2020