92 – ´Abdullaah bin ´Amr amesema:

”´Arshi imezungukwa na nyoka na wahy huteremka katika minyororo.”[1]

[1] Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Haafidhw Ibn Hajar ameashiria Athar hii katika ”al-Iswaabah” wakati alipokuwa anataja wasifu wa al-Bikaaliy na akasema:

”Tumeisimulia katika ”al-Bishraaniyyaat”.”

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Ameipokea Abush-Shaykh katika “al-´Adhwamah”: Muhammad bin al-´Abbaas ametuhadithia: Muhammad bin al-Muthannaa ametuhadithia: Mu´aadh bin Hishaam ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Kathiyr bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Abu ´Iyaadhw, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw. Abu ´Iyaadhw alikuwa akiitwa ´Amr bin al-Aswad. Kisha nikaipata katika ”as-Sunnah”, uk. 150: Baba yangu amenihadithia: Mu´aadh bin Hishaam ametuhadithia…

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 111
  • Imechapishwa: 12/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy