94. Maafikiano ya maimamu kuhusu ujuu na kulingana kwa Allaah

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Ukiongezea kwamba yapo mamia ya maneno, kama si maelfu, kutoka kwa Salaf juu ya hilo. Jengine ni kwamba hakuna katika Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa yeyote katika Salaf si kutoka kwa Maswahabah, waliokuja baada yao wala maimamu wa ummah – walioeshi zama za matamanio na tofauti – herufi hata moja inayoenda kinyume na hayo. Hakuna andiko la wazi kutoka kwao wala kitu cha dhahiri kinachoashiria hilo.

MAELEZO

Maneno ya wanazuoni, yanayotilia nguvu ujuu na kulingana kwa Allaah, ni mengi. Kama maneno yote ya wanazuoni yatakusanywa, basi kungefanywa juzuu kubwakubwa na nyingi. Kwa mfano Imaam Ibn-ul-Qayyim ameandika kitabu kwa jina ”Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah” kuhusiana na mada hii. Wanazuoni wameafikiana kwa njia ya kukata kuthibitisha ujuu na kulingana kwa Allaah – na maafikiano ni hoja ya kukata ubishi. Hakuna herufi hata moja kutoka kwa imamu anayezingatiwa inayopingana na ´Aqiydah hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 136-137
  • Imechapishwa: 28/08/2024