Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Allaah pekee ndiye anayejua kuna dalili ngapi mfano wa hizo. Kuna mapokezi tele, upande wa kimatamshi na kimaana. Zinatoa elimu ya yakini na moja miongoni mwa elimu za lazima ni kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafikishia ummah wake ya kwamba Allaah (Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi na kwamba yuko juu ya mbingu. Allaah amewaumba watu juu ya maumbile hayo watu wote, waarabu na wasiokuwa waarabu, waislamu na makafiri. Isipokuwa tu wale ambao shaytwaan amewatoa katika maumbile yao.

MAELEZO

Elimu ya kilazima ni ile ambayo haiwezi kurudishwa nyuma.

Mapokezi tele yamegawanyika sampuli mbili:

1 – Mapokezi tele upande wa matamshi, kwa njia ya kwamba yamesimuliwa na kundi moja kutoka kwa kundi lingine, kuanzia mwanzo wa cheni mpaka mwisho wake, kwa njia ya kwamba haiwezekani wote wakawa wamesema uwongo.

2 – Mapokezi tele upande wa maana, kwa njia ya kwamba mpokezi mmoja asimulie kupitia njia nyingi na kupitia mapokezi mengi, mpaka maana yake ikapelekea yakini.

Maumbile maana yake ni kuwa Allaah amewaumba viumbe kwa kumtambua na kukubali haki yake pekee ya kuabudiwa, ambapo baadaye baadhi yakaharibiwa maumbile yao na mashaytwaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mtoto yoyote isipokuwa huzaliwa katika maumbile. Baadaye wazazi wake ndio humfanya akawa myahudi, mkristo au mwabudu moto. Ni kama ambavo mnyama huzaa mnyama mzima; je, mtahisi kuwa hana pembe mpaka nyinyi ndiye mumwondoshe pembe?”[1]

Hiyo ina maana ya kwamba kila mtoto huzaliwa juu ya Uislamu. Allaah (Ta´ala) amesema:

فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Umbile la asili la kumpwekesha Allaah ambalo kawaumba watu kwalo; hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah – hivo ndio dini iliyonyooka kisawasawa, lakini watu wengi hawajui!”[2]

[1] al-Bukhaariy (4775) na Muslim (2658).

[2] 30:30

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 135-136
  • Imechapishwa: 28/08/2024