Hadiyth “Atapotawadha muislamu au muumini na akaosha uso wake…”

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

129 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إِذَا تَوَضَّأ العَبْدُ المُسْلِمُ، أَو المُؤمِنُ فَغَسَلَ وَجْهَهُ خَرَجَ مِنْ وَجْهِهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ نَظَرَ إِلَيْهَا بِعَينهِ مَعَ المَاءِ، أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ، فَإِذا غَسَلَ يَدَيْهِ خَرَجَ مِنْ يَدَيهِ كُلُّ خَطِيئَة كَانَ بَطَشَتْهَا يَدَاهُ مَعَ المَاءِ، أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ، فَإِذَا غَسَلَ رِجْلَيهِ خَرَجَتْ كُلُّ خَطِيئَةٍ مشتها رِجْلاَهُ مَعَ المَاء أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ المَاءِ حَتَّى يَخْرُجَ نَقِيًّا مِنَ الذُّنُوبِ

“Atapotawadha muislamu au muumini na akaosha uso wake, litatoka katika uso wake kila dhambi alilolitazama kwa jicho lake pamoja na maji au tone la mwisho la maji. Atapoosha mikono yake, litatoka katika mikono yake kila dhambi alilolishika kwa mkono wake pamoja na maji au tone la mwisho la maji. Atapoosha miguu yake, litatoka katika miguu yake kila dhambi aliloliendea kwa miguu yake pamoja na maji au tone la mwisho la maji mpaka atoke hali ya kuwa amesafika na madhambi.”[1]

Kutajwa kwa jicho ni kwa njia ya kupigia mfano tu na Allaah ndiye anajua zaidi. Kwa kuwa pua pia linaweza kufanya dhambi kwa kunusa mambo ambayo hana haki ya kuyanusa. Vivyo hivyo mdomo pia unaweza kuzungumza maneno ya haramu. Ametaja jicho kwa sababu madhambi mengi yanakuwa kupitia njia ya kutazama. Inatakikana kwa mtu anapotawadha basi ahudhurishe maana hii. Kwa msemo mwingine kutawadha kwake kumsameheshe madhambi yake ili kwa wudhuu’ wake huu aweze kupata ujira kwa Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Muslim

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/182)
  • Imechapishwa: 28/08/2024