94. Haitoshi peke yake kujiepusha na Bid´ah, ni lazima pia kuwakata

Haitoshi kwetu kujiepusha na Bid´ah peke yake. Bali tunatakiwa kuwakata watu wa Bid´ah na tusikae pamoja nao. Hatuwafanyi marafiki mpaka waachane na Bid´ah. Kwa sababu tukiwafanya ni marafiki na kukaa nao tunawashaji´isha juu ya Bid´ah. Kwa hiyo sisi tunawahama kwa maana ya kwamba tunaacha vikao vyao na pia tunaacha kuwafanya ni marafiki mpaka watubie kwa Allaah. Hili ndio jambo la wajibu kwa Ahl-us-Sunnah kwamba wanatakiwa kuwahama Ahl-ul-Bid´ah. Hili lingefanyiwa kazi ipasavyo basi Bid´ah zisingelienea. Lakini wakati watu walipochukulia wepesi kwa wazushi na wanakosa watu wa kuwakemea ndipo wakawa wanaeneza ufisadi juu ya ardhi na kueneza Bid´ah. Wamekuwa ni marafiki zetu na wakazi wetu ndio maana Bid´ah zikawa ni zenye kuenea kwa njia hii. Lakini endapo Ahl-ul-Bid´ah wangelihamwa basi shari yao ingelipungua.

Maneno yake Shaykh:

“Naona kuwahama na kuwatenga Ahl-ul-Bid´ah… “

Kuhama ni kuacha. Kwa msemo mwingine tunaachana nao, kutokaa pamoja nao na kutowafanya marafiki:

“… mpaka watubie.”

 Wakitubia basi Allaah atawasamehe. Tusiwafanye ndio wakazi na wapenzi wetu.

Maneno yake:

“Nawahukumu kwa uinje.”

Bi maana tunawahukumu watu kwa ule uinje wao na hatujui yaliyomo mioyoni mwao. Lakini mwenye kufanya kheri tunamshuhudia kheri kujengea juu ya uinje wake. Mwenye kufanya shari tunamshuhudia shari kujengea juu ya uinje wake. Kuhusu mioyo yao hakuna anayeijua isipokuwa Allaah.

Murji-ah hii leo wanasema kwamba mwenye kufanya kufuru, shirki au maovu basi wewe usimhukumu kwa yale yanayodhihiri kwake. Kwani hujui yaliyomo ndani ya mioyo yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 132-133
  • Imechapishwa: 31/05/2021