92- Haijuzu kuzika katika hali zifuatazo isipokuwa kwa dharurah:

1- Kuzika ndani ya nyakati tatu. Hilo ni kutokana na HAdiyth ya ´Utbah bin ´Aamir iliyotangulia kwa tamko:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anatukataza kuswali au kuwazika maiti zetu ndani ya nyakati tatu; mpaka lichomoze jua kwa kutoa miale yake hadi liinuke, pale linaposimama katikati ya utosi mpaka jua lipinduke na wakati jua linamili kuelekea kuzama mpaka lizame.”

Katika Hadiyth kuna dalili ya wazi juu ya yale tuliyoyataja. Ibn Hazm katika “al-Muhallaa” (05/114-115) ameonelea hivo na wanachuoni wengine.

Miongoni mwa tafsiri zilizo mbali na usawa, bali ambazo ni batili, ni maneno ya baadhi yao: “Maneno yake: “Tuwazika” ina maana ya kuswali.” Abul-Hasan as-Sindiy amesema:

“Haifichikani kuwa ni maana ilio mbali na usawa. Akili haiendani kutokana na tamko la Hadiyth. Baadhi yao wamesema: “Husemwa قبره pindi anapomzika na wala haisemwi hivo pindi anapomswalia.” Kilicho karibu zaidi ni kwamba Hadiyth inaegemea katika maoni ya Ahmad na wengine kwamba imechukizwa kuzika katika nyakati hizi.”

Imaam an-Nawawiy pia ameiraddi tafsiri hii. Lakini lakini katika njia ya kuiendea hilo ametumbukia katika tafsiri nyingine inayofanana na hii na akadai madai ambayo yasiyokuwa imara. Amesema katika “Sharh Muslim”:

“Baadhi yao wamesema kuwa makusudio ya kaburi ni kumswalia swalah ya jeneza, jambo ambalo ni nyonge. Kwa sababu swalah ya jeneza haichukizwi katika nyakati hizi kwa maafikiano. Hivyo haijuzu kuifasiri Hadiyth kwa yanayokwenda kinyume na maafikiano. Bali yaliyo ya sawa ni kwamba maana yake ni kukusudia kuchelewesha mazishi mpaka katika nyakati hizi. Kama ambavo imechukziwa kuchelewesha ´Aswr mpaka kipindi jua linapiga manjanomanjano bila udhuru… Ama kukitokea kuzikana katika nyakati hizi pasi na kukusudia hakuna machukizo.”

Tafsiri hii haina dalili yoyote. Hadiyth hii imetajwa kwa kuachiwa na imekusanya kwa kukusudia na kwa kutokukusudia. Haki ni kwamba ni kwamba haijuzu kuzikana katika nyakati hizo hata kwa ambaye hakukusudia. Yule ambaye swalah ya jeneza itampata kipindi hicho basi asubiri mpaka utapomalizika wakati wa machukizo.

Ama madai yake kwamba swalah ya jeneza haichukizwi katika nyakati kama hizi kwa maafikiano ni kosa kutoka kwake (Rahimahu Allaah). Suala hili wanachuoni wametofautiana. Usawa ni kwamba imechukizwa tofauti na maafikiano inayodaiwa. Imekwishatanguliwa kubainishwa hayo katika masuala ya 89, hali ya kuwa ni mwenye kuyawekea taaliki, uk. 130.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 175-176
  • Imechapishwa: 16/02/2022