90- Katika yale yaliyotangulia wanavuliwa mashahidi waliouliwa katika uwanja wa vita. Wao wanazikwa mahala walipouliwa na wala hawatohamishwa kwenda makaburini. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kutoka al-Madiynah kwenda kwa washirikina ili apambane nao. ´Abdullaah akasema: “Ee Jaabir bin ´Abdillaah! Sioni ubaya wa wewe kutoshiriki Jihaad bali uwe miongoni mwa wale wenye kusubiri khabari ili ujue jambo letu limefikia wapi. Kwani hakika mimi, naapa kwa Allaah, kama mimi ningekuwa sijaacha nyuma wasichana basi ningelipenda uuliwe mbele yangu. Wakati mimi nilikuwa na wale waliobaki tahamaki akaja shangazi yangu akiwa na baba na mjomba wangu akiwa amewafunga kulia na kushoto juu ya ngamia. Akawaingiza katika mji wa al-Madiynah ili awazike katika makaburi yetu. Tahamaki bwana mmoja akaja akiwa ni mwenye kuita: “Zindukeni hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakuamrisheni muwarudishe wale wauliwa na mkawazika sehemu zao walipouliwa. Tukawarudisha na kuwazika mahala walipouliwa.”

Ameipokea Ahmad (03/397-398) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Baadhi yake iko kwa Abu Daawuud na wengineo kwa njia ya mukhtasari. Imekwishatangulia katika masuala ya ya 17, uk. 14.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 175
  • Imechapishwa: 16/02/2022