Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
Inatakiwa vilevile kuamini hodhi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Itaendewa na Ummah wake; hatopatwa na kiu kamwe yule mwenye kunywa humo. Atafukuwa yule ambaye alibadilisha na kugeuza.
MAELEZO
Miongoni mwa mambo yatakayokuwa siku ya Qiyaamah ni hodhi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Itaendewa na Ummah wake na yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atawanywesha kwa mkono wake. Urefu wake ni mwendo wa mwezi na upana wake ni mwendo wa mwezi. Maji yake ni meupe kuliko maziwa, matamu kuliko asali na vikombe vyake ni sawa na idadi ya nyota mbinguni. Yule mwenye kunywa kikombe kimoja basi hatopatwa na kiu tena kabisa. Lakini itatembelewa na watu ambao watafukuzwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atawatambua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atasema:
“Ee Mola wangu! Maswahabah wangu!” Ataambiwa: “Hakika wewe hujui kile walichozua baada yako.”[1]
Waritadi, makafiri, washirikina na wanafiki watafukuzwa mbali na hodhi siku ya Qiyaamah. Hakuna watakaoiendea hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kunywa ndani yake isipokuwa waumini wakweli.
[1] al-Bukhaariy (6211).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 70
- Imechapishwa: 24/08/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)