Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Njia ni haki. Waja watapita juu yake kutegemea matendo yao. Wenye kuokoka inatofautiana kasi ya kusalimika kwao juu yake kutokamana na Moto wa Jahannam. Wako wengine ambao matendo yao yatawafanya kutumbukia ndani.

MAELEZO

Miongoni mwa mambo yatayokuwa ya khatari na hali za siku ya Qiyaamah ni kwamba kutawekwa njia juu ya Moto. Njia ni daraja ambayo ni nyembamba kuliko unywele na yenye makali zaidi kuliko upanga. Watu watapita juu yake kutegemea matendo yao. Wako ambao watapita kama umeme, wengine kama upepo, wengine kama farasi waendao haraka, wengine watatembea kwa miguu yao, wengine watatambaa na wengine watakamatwa  na kutupwa Motoni. Allaah (Ta´ala):

فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَـٰنِ عِتِيًّا ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا

”Naapa kwa Mola wako. Bila shaka Tutawakusanya wao na mashaytwaan, halafu tutawahudhurisha kandoni na Jahannam hali ya kupiga magoti, halafu bila shaka tutawachomoa katika kila kundi wale ambao waliomuasi zaidi Mwingi wa rehema, halafu bila shaka Sisi tunawajua zaidi wale wanaostahiki zaidi kuchomwa humo. Na hapana yeyote katika nyinyi isipokuwa ni mwenye kuufikia.”

Hakuna yeyote isipokuwa ni lazima aipite. Ni lazima kupita juu ya njia hiyo. Kila mmoja ataipita, ni mamoja muumini au kafiri:

فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَـٰنِ عِتِيًّا ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا

”Naapa kwa Mola wako. Bila shaka Tutawakusanya wao na mashaytwaan, halafu tutawahudhurisha kandoni na Jahannam hali ya kupiga magoti, halafu bila shaka tutawachomoa katika kila kundi wale ambao waliomuasi zaidi Mwingi wa rehema, halafu bila shaka Sisi tunawajua zaidi wale wanaostahiki zaidi kuchomwa humo. Na hapana yeyote katika nyinyi isipokuwa ni mwenye kuufikia – hiyo ni hukumu ya Mola wako ambayo lazima itimizwe. Kisha tutawaokoa wale waliomcha Allaah na tutawaacha madhalimu humo hali ya kuwa ni wenye kupiga magoti.”[1]

Kupita juu ya njia ni miongoni mwa mambo yatayokuwa siku ya Qiyaamah. Mtunzi (Rahimhu Allaah) amesema:

“Njia ni haki.”

Bi maana ni lazima kuliamini, kutokana na Aayah hii:

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا

“Na hapana yeyote katika nyinyi isipokuwa ni mwenye kuufikia.”

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameahidi kwamba kila kiumbe ni lazima aufikie Moto; lakini waumini watasalimika nao kutokana na matendo yao na makafiri watatumbukia ndani yake. Kwa sababu hawana matendo mema yatayowavukisha juu ya Njia.

[1] 19:68-72

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 69
  • Imechapishwa: 24/08/2021