92. Athar ”Abu Hurayrah aliulizwa ni vipi tutaswalia jeneza… ”

93 – Abu Musw´ab ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Anas, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Maqburiy, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

”Abu Hurayrah aliulizwa ni vipi tutaswalia jeneza. Akasema: ”Naapa kwa uhai wa Allaah kwamba nitakueleza. Kwanza nalifuata kutokea nyumbani kwake. Pindi linapowekwa chini, huleta Takbiyr, nikamuhimidi Allaah na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

اللهم هذا عبدك، ابن عبدك و ابن أمتك. كان يشهد أن لا إله إلا أنت و أن محمدا عبدك و رسولك، و أنت أعلم به. اللهم إن كان محسنا فزد من إحسانه، و إن كان مسيئا فتجاوز عنه. اللهم لا تحرمنا أجره و لا تفتنا بعده

”Ee Allaah! Huyu ni mja Wako, mtoto wa mja na kijakazi Wako. Alikuwa akishuhudia ya hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wako. Wewe unamjua zaidi. Ee Allaah! Ikiwa alikuwa mwema, basi zidisha katika wema wake na ikiwa alikuwa muovu usimchukulie. Ee Allaah! Usitunyime ujira wake na usitupe mtihani baada yake.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Abu Musw´ab alikuwa akiitwa Ahmad bin Abiy Bakr bin al-Haarith az-Zuhriy al-Madaniy. Ametajwa katika  “al-Muwattwa’” kwa cheni ya wapokezi hii. Yahyaa bin Sa´iyd ameisimulia cheni ya wapokezi kwa njia nyingine pale alipoisimulia kutoka kwa Sa´iyd al-Maqburiy, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye alimuuliza ´Ubaadah bin as-Swaamit kuhusu kumswalia maiti swalah ya jeneza. Ndipo akajibu:

”Naapa kwa Allaah kwamba nitakueleza… ”

Ameipokea al-Bayhaqiy.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 13/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy