91. Athar ”Ibn ´Umar alikuwa akileta Takbiyr katika swalah ya jeneza… ”

92 – ´Abdullaah bin Maslamah ametuhadithia: Naafiy´ bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Nu´aym al-Qaariy’ ametuhadithia, kutoka kwa Naafiy´, ambaye ameeleza:

”Ibn ´Umar alikuwa akileta Takbiyr katika swalah ya jeneza, akimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha anasema:

اللهم بارك فيه، و صل عليه، و اغفر له، و أورده حوض نبيك صلى الله عليه و سلم

”Ee Allaah! Mbariki, msifu, msamehe na mfanye aifikie hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 79
  • Imechapishwa: 13/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy