90. Athar ”Baada ya Takbiyr ya kwanza ya swalah ya jeneza… ”

91 – Muhammad bin Kathiyr ametuhadithia: Sufyaan bin Sa´iyd ametuhadithia: Abu Haashim al-Waasitwiy amenihadithia, kutoka kwa ash-Sha´biy, ambaye amesema:

”Baada ya Takbiyr ya kwanza ya swalah ya jeneza mtu anamsifu Allaah (´Azza wa Jall), baada ya ya pili mtu anamsifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), baada ya ya tatu mtu anamuombea du´aa maiti, baada ya ya nne mtu anatoa Tasliym.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Wapokezi wak wote ni wa al-Bukhaariy na Muslim. Abu Haashim al-Waasitwiy jina lake ni Yahyaa bin Diynaar ar-Ruumaaniy.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 79
  • Imechapishwa: 13/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy