90. Umejiandalia nini kwa ajili ya kaburi lako?

´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) alipokuwa akisimama karibu na kaburi alikuwa akilia sana mpaka ndevu zake zinaloa. Akaambiwa: “Hulii pindi unapofikiria Pepo na Moto na unalia kwa sababu ya hili.” Akasema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kaburi ndio kituo cha kwanza cha Aakhirah. Mwenye kusalimika nayo yote yaliyo baada yake yatakuwa ni mepesi kwake. Asiyesalimika nayo yote yaliyo baada yake yatakuwa magumu.”[1]

at-Tirmidhiy amepokea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sijapatapo kuona muonekano isipokuwa kaburi linatisha kuliko wenyewe.”[2]

Mujaahid amesema:

“Kitu cha kwanza kinachomzungumzisha mwanaadamu ni kaburi lake. Humwambia: “Mimi ndio nyumba ya minyoo. Mimi ndio nyumba ya upweke. Mimi ndio nyumba ya faragha. Mimi ndio nyumba ya giza. Mimi ndio nyumba ya ugeni. Ee mwanaadamu! Haya ndio niliyokuandalia. Wewe umeniandalia nini?”

Abud-Daraa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nisikuelezeni siku ya ufakiri wangu? Ni ile siku nitayoingizwa ndani ya kaburi langu.”

Ja´far as-Swaaqid (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiyatembelea makaburi usiku na kuyaambia:

“Enyi mlio ndani ya makaburi! Kwa nini hamniitikii ninapowaita? Ninaapa kwa Allaah kuwa hawawezi kuitikia. Ni kama mimi ni mmoja katika wao.”

Halafu anaelekea Qiblah mpaka inapoingia alfajiri.

´Umar bin ´Abdil-´Aziyz alimwambia mmoja katika marafiki zake:

“Jana jioni nililifikiria kaburi na mauti. Lau ungeliyaona mauti baada ya siku tatu ungelihisi wasiwasi baada ya kuanasika nayo kwa muda mrefu. Umeona nyumba iliyojaa wanyama. Umeona maji ya majeraha yanayakimbia mauti. Umeshaona minyoo wanavyomla. Harufu imebadilika na sanda imeharibika. Yote hayo baada ya kuwa nzuri, yenye harufu yenye kunukia na iliyo nzuri.”

Kisha akapiga ukelele mpaka akaanguka na kuzimia.

Baadhi ya wenye hekima wamesema:

“Kuna bahari nne ya vitu vinne; mauti ni bahari ya uhai. Nafsi ni bahari ya matamanio. Kaburi ni bahari ya majuto. Msamaha wa Allaah ndio bahari ya madhambi. Tunamuomba Allaah Mtukufu ayafanye makaburi yetu kuwa ni majumba bora kabisa.”

[1] at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na al-Haakim.

[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (1684).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 191-193
  • Imechapishwa: 02/12/2016